Karibu kwenye tovuti ya programu ya Shule Bora

Shule Bora ni programu ya elimu ya Serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa mfuko wa UK aid inayolenga kuinua ubora, ushirikishwaji, na mazingira salama ya kujifunzia kwa wasichana na wavulana wote katika shule za msingi za serikali nchini. Ikitolewa kwa ushirikiano na wizara mbali mbali za serikali, Shule Bora italeta mageuzi ya kudumu yatakayomwezesha kila mtoto kupata mwanzo bora wa elimu, kuendelea hadi shule ya msingi na kumaliza elimu yake, na kuwapa fursa ya kutimiza uwezo wake na kuchangia ukuaji na maendeleo ya nchi.

Ndani ya hii tovuti utakuta habari na nyenzo mbalimbali za kuwezesha uboreshaji wa elimu nchini Tanzania. Nyenzo hizi ni pamoja na matokeo kutoka kwa kazi yetu, zana na taarifa kuhusu utumiaji mbinu bora, takwimu na matokeo/mafanikio ya shughuli za programu. Nimatumaini yetu kuwa taarifa hizi ni muhimu kwako na zaidi kwa wale wanaofanya kazi katika tasnia ya elimu nchini na nje ya Tanzania.

KAGERA KIGOMA TABORA SINGIDA DODOMA MANYARA IRINGA MOROGORO LINDI RUVUMA MTWARA PWANI DAR ESSALAAM TANGA KILIMANJARO ARUSHA SIMIYU MWANZA GEITA MARA SHINYANGA KATAVI RUKWA MBEYA SONGWE NJOMBE
KAGERA KIGOMA TABORA SINGIDA DODOMA MANYARA IRINGA MOROGORO LINDI RUVUMA MTWARA PWANI DAR ESSALAAM TANGA KILIMANJARO ARUSHA SIMIYU MWANZA GEITA MARA SHINYANGA KATAVI RUKWA MBEYA SONGWE NJOMBE