Karibu Kituo cha Taarifa cha programu ya
Shule Bora
Kwa kipindi cha miaka sita, Programu ya Shule Bora imechangia kuleta mageuzi makubwa ya elimu kote Tanzania. Soma na pakua rasilimali, mambo muhimu ya kujifunza na mafaniko ya programu hii hapa. Rasilimali zote

Kuhusu programu
Maendeleo endelevu kwa kila mtoto
Shule Bora ni programu ya miaka sita ya kuimarisha mfumo wa elimu ambayo inalenga kuboresha ujifunzaji kwenye shule za msingi zaidi ya 6,000 nchini Tanzania. Inafadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Idara ya Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Kimataifa (FCDO). Programu hii inatekelezwa kupitia usaidizi wa kitaalam, kwa ushirikiano wa moja kwa moja kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na mamlaka za serikali za mitaa. Inahusisha uwezeshaji wa wataalamu ndani ya mifumo ya elimu ya kitaifa na kikanda, na kuimarisha mifumo iliyopo ya mafunzo ya walimu, elimu jumuishi, pamoja na mipango mkakati inayotumia takwimu. Msisitizo huu wa kuzijengea uwezo taasisi zilizopo ndani ya mfumo wa elimu, unahakikisha kuwa maboresho kwenye mbinu za ufundishaji, ujifunzaji na usalama wa watoto shuleni unakuwa ni endelevu, yanawafikia wengi zaidi , na yanamilikiwa kikamilifu na Serikali ya Tanzania. Kituo hiki cha Maarifa kimekusanya rasilimali zote zilizoandaliwa kupitia programu hii. Kituo hiki cha Maarifa huleta pamoja rasilimali zote zilizoundwa kupitia programu.9
Mikoa
6,000+
Shule zaidi ya zimefikiwa
4
Wanafunzi milioni wamefikiwa
Tsh
bilioni 14.9 zimetolewa kwa Halmashauri/ Mamlaka za Serikali za Mtaa
Kuhusu programu
Uimarishaji wa Mfumo wa Elimu ya Msingi nchini Tanzania
Shule Bora ni programu ya Serikali ya Tanzania inayolenga kuimarisha mfumo wa elimu ya msingi ili kuboresha matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji. Programu hii imewezesha maboresho endelevu kwenye ufundishaji, usalama wa watoto shuleni na matokeo ya ujifunzaji kwa kuchangia kuleta mageuzi ndani ya mifumo ya kitaifa na kikanda, na kuimarisha ushirikiano wa karibu wa kiutendaji kati ya wizara, mamlaka za serikali za mitaa pamoja na wadau wa maendeleo. Kazi hii inatekelezwa sambamba na Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EPforR), ambayo inahusisha Kutoa fedha kulingana na matokeo yanayopimika na kuhakikisha rasilimali zinafika kwenye shule zenye uhitaji zaidi.Washirika wetu
Tumedhamiria kuimarisha elimu nchini Tanzania










