KUHUSU SHULE BORA
Kwa ufadhiri kutoka Serikali ya watu wa Uingereza(UK) kutoka 2021 hadi 2027, Programu ya Shule Bora kitaifa itafanya kazi kusaidia serikali katika programu ya mageuzi ya elimu, na kwa kuboresha elimu katika Serikali za Mitaa na shule za mikoa tisa ya Tanzania yenye changamoto nyingi. Takribani watoto milioni 4, watanufaika na hii programu, nusu yao wakiwa wasichana. Mageuzi na na uvumbuzi vitajaribiwa na kutathminiwa katika ngazi ya mtaa ili mbinu bora zilizothibitishwa ziweze kutumika katika shule zote za msingi nchini.
Kitaifa, Shule Bora hutoa msaada wa kitaalamu kwa serikali kuhusu na kwa programu ya pili ya elimu ya Lipwa Kwa Matokeo yani EpforR II inayofadhiriwa na na wadau mbalimbali. Katika EPforR II, malengo ya utendaji wa kitaifa yanafanyika kwa makubaliano ya pande zote mbiliserikali na wafadhili kuhusu malipo yanayotokana na na mafanikio lengwa. Hii huchochea mabadiliko ya kudumu ya kimfumo kama vile usawa wa usambazaji wa walimu na utoaji wa vitabu vya kiada.
Washirika wetu wakuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MOEST) – Inatoa mwongozo wa kisera na uangalizi matokeo muhimu ya programu.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) – kusimamia utekelezaji katika Mikoa na Halmashauri.
Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) – kutoa mafunzo endelevu ya kitaalamu yenye ubora juu kwa walimu.
Wakala wa Maendeleo ya Usimamizi wa Elimu (ADEM) – Kuboresha usimamizi wa elimu nchini Tanzania
Cambridge Education (CE) ni mshirika wa utoaji wa usaidizi wa kitaalamu kwa Shule Bora. Programu inatekelezwa na washirika wakuu wa Action on Disability and Development (ADD), Plan International, na International Rescue Committee (IRC), na washirika wengine.
Shule Bora imejikita katika matokeo manne;
- Kujifunza: Watoto wote wapo shuleni wanajifunza
- Kufundisha: UK aid inasaidia uimarishaji wa kufundisha kwa walimu wa
Tanzania - Jumuishi: Watoto wote wapo shuleni zenye mazingira salama, yanayovutia
kujisomea na kuwawezesha kumaliza elimu msingi na kwendelea hadi sekondari - Kujenga Mifumo: UK aid inasaidia Serikali kuimarisha thamani ya fedha
zitolewazo kwa elimu shuleni katika ngazi za serikali za mitaa na kitaifa
Ili kufikia matokeo haya. Shule Bora inafanya kazi kutoa
Shule Bora imejikita katika matokeo makuu matano, kila moja ikilenga wadau muhimu tofauti katika kufanikisha matokeo ya programu